Jinsi ya kutoa pesa kwenye akaunti yako
Ili kutoa pesa kwenye Akaunti yako inakupasa kufuata hatua zifuatazo:
Ingia kwenye Akaunti yako (log in) na kisha ubofye sehemu iliyoandikwa
- Akaunti.
- Toa pesa.
- Chagua mtandao husika unaotoka kutolea pesa.
- Weka kiasi cha kutoa (kisipungue Tsh.2000) kisha bonyeza kuendelea.
- Jaza namba yako ya muhamala. (Mfano. +255xxxxxxxxx).
- Bonyeza kuendelea na utoaji wa fedha.
Ili kuweza kufanikisha kutoa pesa kwenye akaunti yako ya Parimatch hakikisha umejaza taarifa zako binafsi.
Ni muhimu pia kuhakikisha umetumia asilimia hamsini (50%) ya kiasi ulichoweka kwenye akaunti yako, kumbuka kuwa mkeka au beti zilizofanyiwa “Cashout” na zile zilizoamuliwa kwa odds ya 1 hazitohesabika katika mahesabu ya asilimia 50%.
Hakikisha huna bonasi inayotumika
Zaidi ya hayo, hutaweza kutoa pesa ikiwa bado una bonasi inayotumika katika akaunti yako. Kamilisha matumizi yote ya bonasi au subiri hadi muda wake wa matumizi uishe kabla hujatuma ombi la kutoa pesa.
Ni muhimu kukumbuka kuwa unahitaji kutumia njia ile ile ya malipo uliyotumia kuweka pesa yako au yoyote nyingine inayopatikana, wakati wa kutuma ombi la kutoa pesa.